Je, wewe unastahiki?

Kiingereza Bora

Maisha Bora


Masomo ya bure ya Kiingereza kwa wahamiaji wapya


Kuhusu Adult Migrant English Program

 • Unapata hadi ya masaa 510 ya masomo ya bure ya Kiingereza na huduma bure ya watoto (kama wanaruhusiwa)
 • Unafunzwa Kiingereza halisi kinachokusaidia kwenye maisha yako mapya, kufanya kazi na kusoma katika Australia
 • Jifunze jinsi ya kufikia huduma za serikali na jamii
 • Pata marafiki wapya ambao walihamia juzi juzi Australia
 • Kuwa tayari kufanya kazi au kusoma na kupanga maisha yako ya kesho


Vigezo vya kuingia

 • Umeisha pata visa ya kuhamia Australkia. Tafadhali jiandikishe kabla miezi sita haijaisha baada ya upokezi wa barua yako ya visa.
 • Umepewa visa ya familia, ya watu wenye ujuzi, ya wakimbizi, ya wanandoa au ya visa za muda zilizokubaliwa*
 • Huwezi kusema/ kusoma / kuandika lugha ya Kiingereza au una haja ya kuboresha Kiingereza chako.
 • Una umri Zaidi ya miaka 18, Baadhi ya vijana wahamiaji wenye umri wa miaka baina 15 na 17 huwenda pia wakastahiki.

*Tafadhali kumbuka kwamba visa zilizokubaliwa kwa muda hazihusishi visa za kazi na likizo, visa za kufanya kazi likizoni au visa za matembezi mafupi.

Njia zingine rahisi za kusoma

 • Kusoma kwa muda wote au kwa muda mfupi katika maeneo kote Queensland
 • Unawungwa mkono na mwalimu wa kujitolea nyumbakni kama huwezi kuhudhuria masomo kwa muda wote
 • Kusomea kwenye mutandao wa kompyuta kupitia kwa mafunzo ya umbali (elimu ya masafa)
 •  Kamilisha AMEP yako kabla ya miaka tano badaa ya kufika nchini Australia


Nitajifunza nini darasani?

 • Jiunge na darasa kulingana na kiwango chako cya Kiingereza.
 •  Ungwa mkono na Maafisa wa ushirikiano wetu kwenye jamii na Kesi Meneja wako wa AMEP wakati unaendelea na masomo.
 • Jifunze kuhusu lugha inaotumiwa kazini hapa Australia, utamaduni na mazoea
 • Pewa masomo ya ziada ya Kiingereza ikiwa umekuwa na elimu ndogo au masuala ambayo anaathiri uwezo wako wakujifunza.
 •  Pewa huduma ya watoto bure wakati unajifunza Kiingereza (chini ya ustahiki)
 • Jiandae kwa ajili ya mahojiano na uandike Resume au CV
 •  Pewa hadi masaa 80 ya uzoefu wa kazi.

Shusha kipeperushi

Unajiandikisha Je?

 

Step 1

Uliza leo

Au

Piga simu: (07) 32445488

Au

Tembelea TAFE Queensland ambayo iko karibu na kwako.
Tafadhali kuwa na maelezo kuhusu pasipoti na visa tayari.

Bonyeza hapa
Step 2

Kamilisha tathmini ya lugha ya Kiingereza na kesi Meneja wa AMEP.
Step 3

AMEP kesi Maneja wako atakuambia darasa lako.

Uliza sasa juu ya masomo yetu ya Kiingereza